Home LOCAL ASKOFU NTUZA AWATAKA WAHITIMU WA KIPAIMARA KUZISHIKA NA KUZIISHI SHERIA ZA KRISTO.

ASKOFU NTUZA AWATAKA WAHITIMU WA KIPAIMARA KUZISHIKA NA KUZIISHI SHERIA ZA KRISTO.


Na: Maiko Luoga, GEITA

Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) Amos Ntuza Novemba 28/2021 alifanya ziara ya kikazi kisha kutoa huduma ya kipaimara katika Achidikonari ya Geita yalipo makao makuu ya Achidikonari hiyo katika Kanisa Anglikana Kristo Mfalme Geita.

Baada ya kuwekea mikono juu yao Askofu Ntuza aliwataka wanafunzi wa Kipaimara kuzishika na kutii amri za Kristo na kuzifuata sheria zake katika kipindi chote cha maisha yao ndani ya Kanisa.

Matika hatua nyingine Askofu Ntuza amewataka waumini wa Dayosisi hiyo kuwa na umoja ili kuweza kuleta maendeleo ya kimwili na kiroho katika Dayosisi ya Victoria Nyanza DVN ikiwemo kupanda makanisa, kuhubiri injili mahali pote na kujenga vitega uchumi vya Dayosisi.

Ibada hiyo Ilihudhururiwa na waumini na Makasisi kutoka maeneo mbalimbali ya Kanisa Anglikana Achidikonari ya Geita, huku wakionesha furaha yao baada ya kusali pamoja na Mhashamu Baba Askofu wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza Amos Ntuza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here