Home SPORTS ZAIDI YA WATU 2000 KUTIMUA VUMBI MBIO ZA ATLAS HALF MARATHON

ZAIDI YA WATU 2000 KUTIMUA VUMBI MBIO ZA ATLAS HALF MARATHON

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

ZAIDI ya watu elfu 2000 wanatarajia kushiriki katika mbio za  Altas  School half  Marathon  2012  inayotarajiwa kuanza Oktoba 14  mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa shule ya Atlsa  Sylivanus Rugambwa anasema kuwa baada ya shughuli ya marathon kukamilika watakuwa na sherehe za mahafali ya 19 ya shule zao za msingi Atlas Madale na Ubungo,Altas Sekondari na Shule za awali.

“Tunategemea kuwa na idadi kubwa ya watu zaidi ya elfu kumi na tano ambao watashiriki katika mahafali hayo katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kamati imejiandaa vyema pamoja na watendaji wake ili kunogesha sherehe hiyo za mahafali na marathon.

Aliongeza kuwa kamati ya utendaji imeandaa siku ya jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi siku ya ukaguzi wa njia ya wakimbiaji ambao watapenda kushiriki watakagua pamoja na njia ya 5km,10km na 21km itakayotumika siku ya Atlas Half Marathon.

Anase.a kuwa katika mbio hizo mgeni ramsi anatarajiwa kuwa waziri mwenye dhamana ya utamaduni,sanaa na michezo  mh.innocent  Bashungwa pamoja na mkuu wa wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe pia kutakuwa na wageni mbalimbali katika mbio hizo.

“Tunategemea mbio zetu zitahughuliwa na watu mbalimbali  wakiwemo wazazi,watoto,wanafunzi mbali mbali wakimbiaji nguli,wakimbiaji wa kawaida  pamoja na makundi maalum,watu mashuhuri viongozi wa serikali” anasema.

Aliongeza kuwa zoezi la usajili wa mbio hizo bado unaendelea katika shule zao  madale na Ubungo kwa kulipia namba 5927380 pamoja na kituo cha mlimani City  kuanzia muda wa saa 2 asubuhi na jioni ya saa 12.

Hata hivyo katika mbio hizo  mshindi wa  kwanza katika mbio za km 21 350,000 ,kilometa 10Km 200,000,5Km100,000.

Mshindi wa pili ni KM21 ni 300,000,10Km ni175,00 5Km ni 75,000,huku mshind  wa tatu ni 21km 200,000,10km 150,000,5Km50,000.

Mshindi wa nne kwa Km 21 ni 150,000, 10Km 10,000,5Km25,000 huku mshindi wa tano 21 Km 100,000 10Km 50,000 huku 5Km15,000.

Previous articleNBC MDHAMINI MKUU WA LIGI KUU TANZANIA BARA.
Next articleMASHABIKI 10000 KUIONA STARS KWA MKAPA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here