Home SPORTS YANGA, AZAM NANI MBABE LEO.

YANGA, AZAM NANI MBABE LEO.

 Na:Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

MABINGWA wa kihistoria  Yanga leo wanashuka dimbani dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa  ligi kuu ya NBC katika mchezo utakaopigwa dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 1:00 usiku. 

Ni mchezo ambao utakuwa na ushindani mkali kutokana na historia ya timu hizi kila zinapokutana.

Hata hivyo vikosi hivi mara nyingi vimekutana hakuna timu iliyoshinda mechi nyingi zaidi ya mwenzake na kwa wastani, kila msimu zimekuwa zikigawana matokeo

Katika msimu uliopita Yanga ilishinda mchezo wa duru ya kwanza na Azam Fc wakashinda mchezo wa duru ya pili.

Hata hivyo huu ni msimu mwingine, Yanga imebadilika lakini hata Azam Fc wamebadilika pia huku kila timu ikihitaji ushindi dhidi ya mpinzani wake.

Wananchi wanasaka ubingwa wa 28 wa ligi kuu baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo, wamedhamiria kutimiza kusudio hilo.

Hata hivyo yanga ili wawe  bingwa wanapaswa kukusanya alama nyingi kuliko wengine wote na muhimu unapaswa kupata alama nyingi dhidi ya wapinzani wako katika mbio za ubingwa.

Hivyo ni mchezo ambao Yanga inahitaji kuondoka na alama zote tatu pamoja na kuwa hautakuwa mchezo mwepesi

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wachezaji wako tayari na wanajua aina ya mchezo wanakwenda kucheza dhidi ya Azam Fc

Kwa upande wa kocha wa  Azam FC, George Lwandamina amesema kwa sasa malengo yao ni kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuondoshwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

“Upungufu uliojitokeza umetupa funzo kuelekea michezo yetu ijayo, naamini kutokana na ushiriki huu tumepata mwanga wa kikosi changu kufanya vizuri,” alisema.

Amesema  kuwa mchezo wao na Yanga huwa mgumu siku zote ila wamejiandaa vyema kuibuka na ushindi baada ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo.

“Ninachokifanya ni kuwapa wachezaji wangu mbinu za kuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri, kila timu imejipanga hivyo lazima kukabiliane na changamoto za aina yoyote,” alisema.

Winga mshambuliji wa timu hiyo Idd Seleman ‘Nado’ alisema kuwa kutolewa kwao kumewaongezea ari na hamasa ya kupambana zaidi.

Previous articleASASI ZA KIRAIA NI CHACHU KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU- WAZIRI GWAJIMA
Next articleMEYA KUMBILAMOTO AWATAKA MADIWANI WENYEVITI ILALA KUACHA NONGWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here