Home LOCAL WAZIRI GWAJIMA ASHIRIKI UZINDUZI WA KITUO CHA UDHIBITI WA MAGONJWA NCHINI KENYA

WAZIRI GWAJIMA ASHIRIKI UZINDUZI WA KITUO CHA UDHIBITI WA MAGONJWA NCHINI KENYA


Na. WAMJW-Nairobi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima mapema leo ameshiriki mkutano wa uzinduzi wa kituo cha kanda ya mashariki mwa Afrika kinachoshughulikia udhibiti wa magonjwa (EA Regional Collaboration Centre) kinachosimamiwa na kituo cha udhibiti wa magonjwa Afrika (Afrika CDC).

Kituo hiki kinaratibu na kuimarisha udhibiti wa magonjwa ya milipuko na yale yenye umuhimu katika jamii na kinatarajiwa kujengea uwezo wataalam wa afya ya jamii,kuimarisha taasisi za kitaifa za afya ya jamii, kuanzisha mtandao wa kikanda wa ufuatiliaji wa magonjwa na huduma za kimaabara pamoja na kuimarisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa za afya.Kituo cha EARCC kinajumuisha nchi 14 ambazo ni Tanzania, kenya , Uganda ,Rwanda, Burudi, DRC, South Sudan, Djiobut, Sudan, Somalia, Comoro, Sychalles, Madagascar ,Eriteria na Ethiopia.

Uanzishwaji wa kituo hiki unafuatia maazimio ya wakuu wa nchi za Afrika walipokutana kwenye kikao cha mwaka 2015.

Previous articleTAMKO LA THBUB WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI, OKTOBA 1, 2021
Next articleMAJALIWA: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO UNAOTOLEWA NA TAASISI ZA KIDINI NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here