Home SPORTS WAOGELEAJI NANE KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFRIKA GHANA.

WAOGELEAJI NANE KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFRIKA GHANA.

 
Na: Stella kessy.
JUMLA ya  waogeleaji  nane wanatarajia kuondoka kesho asubuhi kuelekea Ghana katika mashindano ya Afrika.

Akizungumza leo na waandishi wa habari  mwenyekiti  wa chama cha kuogelea  nchini Iman Domick  amesema kuwa wachezaji wamejiandaa vya kutosha.

“Vijana wamejipanga vya kutosha katika kuhakiksha wanafanya vyema ili kuitangaza vyema Tanzania  kwani sina shaka na wachezaji wangu nina imani na maandalizi wao ambayo wamefanya “alisema.

Hata hivyo katika michuano hiyo zipo nafasi tatu huku kwa Tanzania wamepeleka nafasi mbili nazo  ni junior Champion ship na Senior champion ship.

Aliongeza kuwa jumla ya wachezaji 8 ambao wataenda kushindana ni watano wanaume na wanawake watatu.

Anasema kuwa  michuano hiyo inaanza tarehe 11-17 Oktoba na watapumzika na vya kutosha na kuanza michuano hiyo.

Alifafanua kuwa katika mchezo huo wazazi wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha watoto wao na  kuongeza morali.

Alitoa mwito kwa watanzania pamoja na wadau mbalimbali kuwekeza katika mchezo huu ambao una nafasi kubwa katika kuinua Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here