Home BUSINESS WADAU WA UTALII MKOANI ARUSHA WAJADILI NAMNA YA KUBORESHA SEKTA HIYO

WADAU WA UTALII MKOANI ARUSHA WAJADILI NAMNA YA KUBORESHA SEKTA HIYO

Mkurugenzi wa hotel ya Masailand iliyopo mjini hapa,Dokta Charles Bekon akizungumza  na waandishi wa habari  katika warsha hiyo ya wadau wa utalii iliyofanyika mjini hapa (Happy Lazaro).
 

Mkurugenzi wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF),Zachy Mbenna akizungumza katika warsha ya wadau wa utalii iliyofanyika jijini Arusha.(Happy Lazaro).

Happy Lazaro, Fullshangwe Arusha.

Arusha.Wadau mbalimbali wa  sekta ya utalii mkoani Arusha wamekutana na kujadiliana namna ya kuweza kuboresha sekta ya utalii na kuweza kuutangaza utalii wetu ndani na nje ya nchi.
 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Zachy Mbenna wakati akizungumza katika warsha iliyofanyika mkoani hapa na kuwashirikisha wadau hao katika kujadili namna ya kuweza kuboresha sekta hiyo na kutangaza vivutio vyetu .
 

Amesema kuwa, sekta ya utalii nchini ni sekta muhimu sana ambayo inatakiwa kutazamwa kwa karibu kwa kuwanoa na kuwapatia mafunzo wadau wake ili kila siku wapate jambo jipya la kuboresha katika utendaji kazi wao.
 

Mbenna amefafanua kuwa,kupitia warsha hiyo pia wanapewa mafunzo namna ya  kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili waweze kujenga uchumi shirikishi ambao utaweza kuhudumia ndani na nje ya Afrika Mashariki.
 

“mafunzo haya tunayotoa kwenye warsha hii yatawasaidia  pia kuyatumia kwenye maonyesho  ya utalii kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika  jijini Arusha ambapo wadau watapata fursa mbalimbali za kuweza kujifunza na hata kuutangaza utalii kwa njia mbalimbali ,hivyo warsha hii wanapata mbinu mbalimbali za kuweza kutangaza utalii wetu pia.”amesema .
 

Mbenna ameongeza kuwa, wadau hao wanajengewa uwezo pia namna bora ya kuweza kujishughulisha na ujasiriamali na kuweza kupambana na biashara zao na kuwa endelevu hasa katika kipindi hiki ambacho nchi imekumbwa na janga la ugonjwa wa COVID ambapo limeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii.
 

”Bado wadau wengi wana changamoto kubwa  katika swala la majadiliano ya kibiashara na wengi wao  wanakosa ubunifu na maarifa katika kufanya majadiliano hayo hivyo kupitia warsha hii leo wadau wetu watatoka hapa na uelewa mkubwa zaidi tofauti na waliokuwa nao.”amesema Mbenna.
 

Naye Mdau wa utalii Dokta Charles Bekon amesema kuwa, wanaishukuru taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine katika kuwaletea mafunzo hayo ambayo wanafundishwa mbinu bora za kuinua utalii wao ili waweze kuutangaza ndani na nje ya nchi .
 

Dokta Bekon amesema kuwa,kupitia mafunzo hayo watapata fursa ya kujifunza mbinu na namna  bora za kuweza kutumia kutangaza utalii hasa katika maonyesho ya utalii  yanayofanyika  jijini Arusha ambayo ni fursa kubwa Sana kwa mkoa wetu na nchi kwa ujumla katika kutangaza utalii wetu.
 

“Tunaishukuru Sana Serikali kwa kutuletea maonyesho hayo hapa mkoani Arusha na sisi tunamwahidi Rais wetu kuwa tumejiandaa vizuri Sana kama wadau wa utalii katika kutangaza nchi yetu na vivutio mbalimbali vilivyopo na kuweza kuwa mfano wa kuigwa.”amesema Dokta Bekon.
 

Kwa upande wake Muongoza watalii mwanamke ,Hosiana Siao amesema kuwa,kupitia mafunzo hayo yanawajengea uwezo namna ya kuweza kutangaza utalii ndani na nje ya Afrika Mashariki huku wakitumia mbinu bora za kuweza kuwashawishi watalii kuvutiwa na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini na hatimaye utalii kuweza kuongezeka na kuinua kipato cha nchi.
Credit – Fullshangwe Blog.

Previous articleMKURUGENZI ARUSHA DC: WAZAZI ACHENI KUWAGEUZA WATOTO WA KIKE KUWA KITEGAUCHUMI CHA FAMILIA.
Next articleTANZANIA, (AFASU) YASAINI MAKUBALIANO KUWEZESHA NA KUKUZA UWEKEZAJI, BIASHARA NA UTALII NCHINI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here