Home SPORTS WACHEZAJI STARS FULL MZUKA KUIKABILI BENIN KESHO

WACHEZAJI STARS FULL MZUKA KUIKABILI BENIN KESHO

Na: Stella Kessy.

MENEJA wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema wachezaji wote wamewasili na wana morali ya ushindi katika mechi ya kesho dhidi ya Benin utaochezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa, jijini Dar es salaam.

Amesema kulingana na wapinzani wao (Benin) kuwa na kikosi imara huku nyota wengi kucheza soka balani Ulaya  ana imani mechi itakuwa ya ushindani mkubwa kwa kila upande kutafuta point.

“Sisi na Benin tumepishana magoli lakini pointi zipo sawa katika kundi, ninawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuongeza sapoti kwa wachezaji pindi kikosi kikiwa uwanjani” amesema.

Aliongeza kuwa  wachezaji wana morali ya kutosha kuhakikisha wanashinda mchezo huo, ili kuwapa nguvu yakujiandaa vyema dhidi ya Benin.

“Wachezaji wana hamu kucheza mechi hiyo, ingawa kocha ndiye anajua nani atacheza kutokana na kiwango watakachokionyesha katika mazoezi yao ambayo  tumeanza  jana”anasema

“Wachezaji wapo vizuri, naamini watafanya vyema ingawa tunaiheshimu Benin ina wachezaji wazuri” ameongeza

Previous articleMAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AZUNGUMZA NA JUMUIYA YA WANAWAKE UWT MKOA WA DAR ES SALAAM
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TANO OCT.6 -2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here