Mwandishi wetu.
TIMU ya taifa ya wanawake, Twiga Stars imetinga na kuingia Fainali ya Kombe la COSAFA baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa Nelson Mandela Bay Jijini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Mabao ya Tanzania leo yamefungwa na Deonisia Minja dakika ya sita na Mwanahamisi Omary dakika ya 79 na kwa matokeo hayo Twiga Stars inafikisha pointi sita kufuatia kuichapa na Zimbabwe 3-0 kwenye mechi ya kwanza Jumatano.
Beki Famta Issa ‘Densa’ amechaguliwa Mchezaji wa Bora wa mechi hiyo kama ilivyokuwa kwenye mechi ya kwanza Mwanahamisi Omary alishinda tuzo hiyo dhidi ya Zimbabwe.
Twiga Stars inayofundishwa na kocha Bakari Shime itakamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Sudan Kusini Jumatatu.