Home SPORTS TWIGA STARS KAMA MLIVYOSIKIA

TWIGA STARS KAMA MLIVYOSIKIA

Na: Mwandishi wetu

TIMU ya Taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars leo  imetupwa nje katika mbio za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchapwa 3-2 na Namibia katika Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Huku mabao ya Namibia  yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Zenatha Goeieman Coleman yote matatu.

Na upande wa  Twiga Stars yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Chabab Atlas Khenifra ya Morocco Mwanahamisi Omary Shaluwa ’Gaucho’ na mshambuliaji wa Simba Queens, Opa Clement Sanga.

Hata hivyo Twiga Stars inatolewa kwa jumla ya mabao 5-3 baada ya kuchapwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa awali  mabao ya Namibia yote yalifungwa na Coleman, wakati bao pekee la Twiga Stars lilifungwa na kiungo wa JKT Queens, Stumai Abdallah Athumani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here