Home SPORTS THADEO LWANGA ASHINDWA KUIZUIA FURAHA YAKE

THADEO LWANGA ASHINDWA KUIZUIA FURAHA YAKE

Na: Mwandishi wetu.

KIUNGO mkabaji Taddeo Lwanga ameweka wazi furaha yake ya kufunga bao muhimu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika katika ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana mchezo Uliopigwa Botswana.

Taddeo alifubga bao hilo dakika ya pili baada ya walinzi wa Jwaneng kuzembea kuondoa mpira wa kona uliopigwa na kiungo Rally Bwalya.

Kiungo huyo raia wa uganda amesema anaamini ataendelea kifunga na kuisaidia Sinba kupata matokeo endapo atapata nafasi ya kufanya hivyo.

“Kama mchezaji najisikia furaha kufunga kwenye michuano mikubwa kama hii na kuisaidia timu kupata ushindi ugenini,binafsi naamini nitaendelea kufunga kama nikipata nafasi’amesema.

Licha yabkuwa na mtaji mzuri na mabao mawili ya ugenini Taddeo amesema bado hawatakiwi kuwachukulia poa Galaxy katika machezo wa marudiano wiki ijayo kwani wana timu nzuri na kwenye soka lolote linawezekana

“Galaxy siyi timu mbaya wako vizuri bado tunapaswa kuhakikisha tunachukua tahadhari ili kupata ushindi wiki ijayo kufuzu hatua ya makundi ya michuano na hilo ndio lengo letu” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here