Home LOCAL TGNP YAZUNGUMZIA MAFANIKIO MAKUBWA WALIYOPATA KUIFIKIA JAMII NA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO.

TGNP YAZUNGUMZIA MAFANIKIO MAKUBWA WALIYOPATA KUIFIKIA JAMII NA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi akizungumza na wadau WA Asasi za kiraia kwenye mkutano maalum ulioandaliwa na TGNP Kueleza mafanikio makubwa waliyoyapata katika kuifikia jamii ya watanzania kwa kupitia dhana ya ujenzi wa nguvu za pamoja katika kuleta mabadiliko.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi amesema kuwa jamii ya watanzani ina wajibu wa kupaza sauti zao katika kuibua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao ili zifanyiwe kazi na kupatiwa ufumbuzi.

Ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Asasi za Kiraia kuweza kusikia ni namna gani TGNP imeweza kuifika jamii na kuweza kuibua changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yao na kuzifanyiakazi kwa kushirikiana na viongozi wa eneo husika.

Amesema TGNP imekuwa ikifanya uchambuzi wa kina juu ya masula mbalimbali ya kijamii nakwamba jamii husika kusikika kwa kupaza sauti ikiibua changamoto mbalimbali zitokanazo na uchambuzi huo nakwamba kwa kufanya hivyo kunaiwezesha jamii hizo kuweza kufikiwa na kutambuliwa.

“Tunataka Sauti isiwe ya TGNP, sauti iwe ya wanajamii tunataka hizi ajenda wazibebe wao kama wanajamii, wazifanyie kazi wao kwenye ngazi zao na ngazi ya kitaifa tunachotaka ni kusikia ajenda sio kusikia sauti ya mtu mmoja kwenye Shirika au watu wachache” Amesema Liundi.

Kwa upande wao baadhi ya wadau wanaofanyakazi za kijamii kwa kushirikana na TGNP wamezungumzia umuhimu wa dhana ya ujenzi wa nguvu za pamoja katika kuleta mabadiliko kwa jamii, wamesema kuwa Shirika hilo la TGNP limekuwa msaada mkubwa kwao kuweza kuifikia jamii inayowazunguka na kutoa elimu mbalimbali za masula ya kijinsia kwa kuandaa vipaumbele vyao na kuviwasilisha kwenye ngazi ya uongozi.

“Baada ya kufanya tafiti ndogo sisi kama wanajamii tuliweza kupeleka mapendekezo kwenye Baraza la Madiwani kwaajili ya kudai halmashauri itenge fedha kwaajili ya mtoto wa kike, mara ya kwanza ilikubali wakatenga milioni 1.6, lakini mpaka sasa wametenga zaidi ya milioni 7, pia tuliweza kupeleka taulo za kike kwenye shule mbalimbali baada ya kubaini kuwa kumekuwa na mahudhurio madogo shuleni kutokana na shangamoto hii”ameeleza Bi. Flora Mlowezi, Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na Maarifa halmashauri ya Mbeya.

“Pamoja na Serikali kuwa na Sera nzuri ya elimu kwa wototo wote lakini wenzetu walituletea mazingira magumu kwa watoto wa  kike, Baraza ikabidi tuchukue hatua ambayo imepelekea kujenga mabweni tisa kwenye Shule tisa lakini pia tukaona tuwe na shule moja ya kiwilaya hivyo tukapitisha bajeti kutoka kwenye vyanzo vya ndani ambayo mwakani inaingiza kidato cha nne na kizuri zaidi ni kwamba tuna tarafa tatu tunahitaji kwenda kila tarafa kujenga shule nyingine kwa sababu matokeo ya wale watoto yalikuwa mabaya sana kielimu, lakini sasa wamepata Divisheni II, Divisheni III, kutokana na mazingira mazuri ya kusomea tofauti na huko nyuma ambapo walikuwa wanapata Divisheni IV, au 0” Ameeleza Mwalimu Kusemba, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.  “Nilianza kama mshiriki wa semina za jinsia na maendeleo pale TGNP baada ya kuelewa masuala ya jinsia nikaamua kuwashawishi wenzangu kule kipunguni na kuanzisha kituo cha taarifa na maarifa ambapo niliweza kuhamasisha wana jamii ya kipunguni kuachana na mila potofu ya kukeketa watoto wa kike na wasichana wadogo ambapo mwanzo ilikuwa ni ngumu lakini mpaka sasa hivi jamii ile ile ndio inayoshiriki elimu ya kuzuia vitendo hivyo” amesimulia mwana harakati Selemani Bishagazi.

Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP ni miongoni mwa Mashirika yaliyoshiriki Wiki ya AZAKI inayofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuwaleta  kwa Pamoja  wadau wakuu wa maendeleo  ikiwemo Serikali, Sekta binafsi na Asasi za Kiraia  Pamoja na wananchi kwa lengo la  kujadili masuala yanayohusu  ustawi wa  nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla inayotarajiwa kufungwa rasmi Octoba 28, Mwaka huu.

ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI ZA MKTUNO HUO ULIOFANYIKA ROYAL VILLAGE JIJINI DODOMA.






Previous articleWAZAWA WA MARA WATAKIWA KUWEKEZA KWAO.
Next articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI OCTOBA 28-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here