Home SPORTS TANZANIA SHOTOKAN KARATE YANG’ARA CONGO

TANZANIA SHOTOKAN KARATE YANG’ARA CONGO




Na: Mwandishi Maalum, DRC.

TIMU ya Taifa ya Mchezo wa Shotokan Karate ya Tanzania imeng’ara katika mashindano ya kimataifa ya Karate kwa Nchi za Maziwa Makuu yaliyofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuanzia tarehe 23 na kumalizika 24 Octoba, 2021. 

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Msaidizi Hidhaifa Hassan  amesema kuwa ujumla wamepata medali 27 kwa categories tofauti tofauti ambapo wanawake wameleta medali 13 na wanaume ni medali 14.

“Katika medali hizo tuna Gold 7, Silver 8 na Bronze 12.” Timu hiyo iliondoka nchini kupitia Rwanda baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara yenye dhamana na Michezo kukwamua changamoto ya usafiri na vibali kwa ajili ya Timu hiyo kuvuka kupitia mpaka wa Rwanda uliokuwa umefungwa,”alisema Katibu wa Chama hicho Hudhaifa.

Aliongeza kuwa timu hiyo inatarajia kurejea nchini ya tarehe 27 Octoba, 2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here