Home BUSINESS TANZANIA KUENDELEA KUNUFAIKA NA SHIRIKA LA MILIKI UBUNIFU DUNIANI

TANZANIA KUENDELEA KUNUFAIKA NA SHIRIKA LA MILIKI UBUNIFU DUNIANI

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa akiwasilisha taarifa ya Nchi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Nchi Wanachama wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) unaofanyika Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 4 hadi 8 Oktoba, 2021.
 
GENEVA USWISI.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa amesema Tanzania itaendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO).

Ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Nchi Wanachama wa WIPO ulioanza tarehe 4 Oktoba na utahitimishwa tarehe 8 Oktoba, 2021 katika Mji wa Geneva, Uswisi

Katika hotuba yake, Bw. Nyaisa amebainisha miradi ya Miliki Bunifu ambayo nchi ya Tanzania imenufaika ikiwemo kujengea uwezo makundi mbalimbali ili kuweza kutumia Miliki Bunifu kwa maendeleo ya nchi. 

“Mpaka sasa BRELA  imeweka mfumo wa kushughulikia maombi ya hataza na alama za biashara (IPAS), mapitio ya sheria za Miliki Bunifu pamoja na vitabu na  ufundishaji wa sehemu ya Shahada ya Uzamili ya Miliki Bunifu inayotolewa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam,” ameeleza

Ameongeza kwa kusema kuwa, hivi karibuni WIPO na Mahakama ya Tanzania wamesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kwa nia ya kuimarisha mfumo wa mahakama na huduma za Miliki Bunifu na ulinzi nchini Tanzania. Utekelezaji wa makubaliano hayo utasaidia kushughulikia changamoto za kisheria zinazohusiana na uamuzi wa Miliki Bunifu unaokabili mfumo wa Mahakama nchini Tanzania

Mkutano huo utapitia na kujadili shughuli mbalimbali na kupitisha bajeti ya WIPO. Tanzania imekuwa mwanachama wa WIPO tangu mwaka 1983.

Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano- BRELA

Previous articleRAIS SAMIA AELEKEZA KUPUNGUZWA TOZO KWENYE MAFUTA
Next articleMEMBE – RAIS SAMIA ANATOSHA KUIONGOZA TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here