Home SPORTS STARS YAPOTEZA NYUMBANI 1-0 DHIDI YA BENIN

STARS YAPOTEZA NYUMBANI 1-0 DHIDI YA BENIN

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Stars leo imepokea kichapo  kwa Benin katika mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe  La Dunia 2022 nchini Quartar,  katika mchezo uliopigwa dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi cha kwanza  timu zote zilipambana lakini  hakuna timu iliyofanikiwa  kuona lango la mwenzie.

Katika dakika za  70 aliyefunga bao ni  steven  Mounie  ambaye alipachika  kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

Huku jitihada za Stars kupata bao zilikwama ambapo mshambuliaji John Bocco alikosa nafasi ya wazi akiwa ndani ya 18 kwa kushindwa kufunga baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa Benin.

Ni mchezo wa kwanza Stars kupoteza katika kundi J na wanapoteza pointi tatu wakiwa katika Uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wake.

Kwenye msimamo sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na vinara ni Benin wenye pointi 7.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here