Home SPORTS STARS YAIFUATA BENIN MCHEZO WA MARUDIANO

STARS YAIFUATA BENIN MCHEZO WA MARUDIANO

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania leo wameifuata  Benin kwenye mchezo wa marudiano kufuzu Kombe la Dunia.

Stars jana wamepoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Benin mchezo uliopigwa  Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2021 nchini Benin ikiwa ni vita ya kusaka pointi tatu muhimu.

Taifa Stars itaondoka na Ndege ya Air Tanzania leo na ina matumaini makubwa ya kuweza kupata ushindi licha ya kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kusema kwamba walipata nafasi na kushindwa kutumia ambazo walizipata.

“Tulishindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata hivyo kwa ajili ya mchezo wetu ujao tutapambana kufanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu,” 

Kwenye Kundi J vinara ni Benin wakiwa na pointi 7 huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake ni nne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here