Home SPORTS SIMBA YATAKATA BOTSWANA YAICHAPA GALAXY 2-0

SIMBA YATAKATA BOTSWANA YAICHAPA GALAXY 2-0

Na: Mwandishi wetu.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara  Simba leo  wameibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy katika  michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza  uliopigwa  Botswana.

Simba ilianza kupata bao la kwanza dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa kiungo wake  Taddeo Lwanga aliyepiga shuti kali baada ya mpira wa kona uliopigwa na Rally Bwalya na kimalizia na John Bocco.Katika dakika ya 6 simba ilifanikiwa kuongoza   bao la pili lililofungwa na nahodha wa timu hiyo John Bocco.

Baada ya mabao hayo mawili ya mapema, Galaxy walianza kutafuta mabao ya kusawazisha lakini walijikuta wakikwama kwenye ukuta wa Simba uliokuwa unalindwa  mabeki.

Matokeo hayo yanakuwa na faida kubwa kwa Simba kwani Jwaneng watakuwa na kibarua kizito cha kupindua matokeo wakati watakapokuja kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Octoba 24, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here