Home SPORTS SIMBA SC YADONDOKEA SHIRIKISHO

SIMBA SC YADONDOKEA SHIRIKISHO

Na:Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara  Simba SC leo wamechezea kichapo 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy katika  michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika mchezo uliopigwa  jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika matokeo ya jumla yanakuwa 3-3 kufuatia Galaxy kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Jijini Gaborone, lakini Simba SC inatolewa kwa kuruhusu mabao zaidi nyumbani.

Hata hivyo katika mchezo wa leo Simba ilianza vyema mchezo wa leo kwa bao la kiungo Mzambia, Rally Bwalya dakika ya 41, lakini Galaxy ikazinduka kipindi cha pili kwa mabao ya Rudath Wendell dakika ya 46 na 59 na Gape Mohutsiwa dakika ya 86.

Wakati Galaxy inatinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa, Simba itakwenda kumenyana na moja ya timu za Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi pia ya michuano hiyo midogo ya CAF.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here