Home SPORTS SIMBA KAMILI GADO KUIVAA GALAXY LEO.

SIMBA KAMILI GADO KUIVAA GALAXY LEO.

Na: Stella Kessy.

KIKOSI cha simba leo wanashuka dimbani kuchuana na Jwaneng Galaxy katika michuano ya klabu bingwa Afrika  msimu wa 2021/2022 katika mchezo utakaochezwa nchini Botswana. 

Katika mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa taifa wa Botswana  utaanza saa 9 lakini kwa saa ya hapa nchini ni saa 10 jioni.

Hata hivyo kikosi kilifika salama na kufanya mazoezi ya kujiweka sawa katika mtanange wa leo.

Pia maandalizi ya mchezo huo yamekamiki  kwa asilimia 100 na wachezaji wote 24 waliosafiri wapo Kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo.

Akizungumza kocha Mkuu Didier Gomes amesema kuwa  katika msimu huu wamelenga kufika katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa  na ili waweze kitimiza ndoto zao ni lazima wafanye vyema katika mchezo wa leo ili iwe rahisi katika mchezo wa marudiano.

“Tunajua haitakuwa mchezo rahisi  Galaxy ni timu inayocheza kwa kishambulia lakini mazoezi tuliyokuwa nayo tutahakikisha tunapambana kupata matokeo mazuri” amesema Gomes.

Kwa upande wa Nahodha John Bocco amesema kuwa kikosi kipo tayari kupeperusha bendela  huku kila mmoja atahakikisha anajitoa kwa asilimia zote ili kuleta ushindi.

Katika mchezo huo wa leo kikosi cha simba kitawakosa wachezaji wao nyota Jonas Mkude,Abdul Swamad Kassim na Ahmed Feruz  ambao wamebaki jijini Dar es Salaam kisubiri mechi ya marudiano.

Huku mshambuliaji Chriss Mugalu  na kiungo Pape Ousmane Sakho wao hawajusafiri na kikosi kutokana na kuendelea kuuguza majeraha ingawa wako mbioni  kurejea dimbani.

Huku kwa upande wa nyota wengine Kibu Denis na Yussufu Mhilu wamebaki  Dar es Salaam kutokana na kuchelewa kupata kibali kutoka Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) hivyo nao watacheza katika hatua inayofuata

Previous articleZOEZI LA MABADILIKO YA HADHI YA VYETI VYA USAJILI WA JUMUIYA ZISIZO ZA KIDINI KATIKA MIKOA YA SHINYANGA, GEITA, MWANZA, MARA, KAGERA NA SIMIYU
Next articleMARWA AIBUKA KIDEDEA CHANETA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here