Mwandishi wetu
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha kwa niaba ya Serikali amewapa moyo wachezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa miguu U 20 (Tanzanite) kuwa Serikali iko pamoja nao wapambane ili kufika kombe la dunia,
Ameyasema hayo jioni ya leo Octoba 08, 2021 wakati alipoitembelea timu hiyo ikiwa mazoezini Uwanja wa Uhuru kujiandaa na mechi yao ya marudiano na Timu kutoka Eritrea kesho jioni katika Uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es salam.
“Nami nawahakikishi watanzania wote wapo karibu nanyi lakini pia raisi anafurahishwa na jitihada zenu kwa wanawake kionekane nanyi mnamuonesha kweli, jana Taifa stars imetuhuzunisha lakini tukapoozwa na twiga stars, Serikali tunawatakia kila la kheri mechi ya kesho nanyi mtupe nguvu zaidi,”alisema Msitha.
Aidha, Msitha amewaahidi kuwa baada ya kumaliza mechi yao kuna zawadi Serikali imewaandalia kuwakabidhi kama ilivyofanya kwa Timu ya wakubwa ya Twiga Stars ili kiwasaidie kukidhi mahitaji yao madogo.
Kwa upande wake Nahodha wa Tanzanite Irene Elias ameahidi Serikali na watanzania wote kuwa nia ya timu yake siyo kufanya vizuri katika mechi ya kesho na Eritrea tu bali kufika Kombe la dunia.