Home LOCAL “SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA WAHARIRI ,VYOMBO VYA HABARI UELIMISHAJI CHANJO...

“SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA WAHARIRI ,VYOMBO VYA HABARI UELIMISHAJI CHANJO YA UVIKO-19”

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Gerson Msigwa akizungumza katika semina hiyo.
 



Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika semina hiyo.

Na:Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amewapongeza wahariri na vyombo vya habari nchini kwa jitihada wanazofanya Katika kuhabarisha Umma juu ya chanjo ya UVIKO-19.

Msigwa ameyasema hayo Leo wakati wa warsha ya wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika Leo jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa katika kipindi Cha wiki mbili wahariri hao pamoja na vyombo vyao vya habari wameweza kufanya juhudi kubwa na kwa wiki mbili matunda yameonekana.

“Kazi kubwa ambayo imefanywa na wahariri na vyombo vyao imesaidia kwa kiasi kikubwa ,niwapongeze sana kwani matokeo tunayaona”.Aliwapongeza

Hata hivyo Msigwa ametoa wito kwa wananchi ambao hawajaweza kuchanjwa wajitokeze kwani takwimu zinaonesha wale ambao hawajachanjwa ndio wanaokuwa Kwenye Hali mbaya mara wapatapo MAAMBUKIZI ya UVIKO-19.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi kitengo Cha elimu ya afya kutoka Wizara ya Afya Dkt.Amalberga Kasangala amesema kuwa suala la kuelimisha ni mtambuka na hivyo inahitaji wataalam mbalimbali Katika kuwaelimisha wananchi.

“Katika kufanikisha hili wizara inashirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na wadau wengine wa Maendeleo na kuhakikisha chanjo zote zinazoingia hapa nchini Zina usalama.

Dkt.Amaberga amesema kuwa Wanahabari wapo Katika hatari ya kupata maambukizi kulingana na mazingira wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hata hivyo amewataka wahakikishe wanaendekea kuwaelimisha wananchi kupata chanjo na wao wanachukua kinga ikiwa ni pamoja na kupata chanjo hiyo.

Previous articleMBUNGE BONAH APOKEA KERO YA MIKOPO KISURU
Next articleTIMU YA MAWAZIRI NANE YATUA RASMI SINGIDA NA UJUMBE WA RAIS SAMIA KWENYE MAENEO YENYE MIGOGORO YA ARDHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here