Home LOCAL RC MAKALLA: DAR SUNSET CARNIVAL KUPAMBA MOTO COCO BEACH KESHO.

RC MAKALLA: DAR SUNSET CARNIVAL KUPAMBA MOTO COCO BEACH KESHO.

 

– Asema Maandalizi yote yamekamilika.

– Burudani za kila aina zitapatikana kesho.

– Asema ni sehemu sahihi na Salama kwa mtoko wa kifamilia.

Na: James Lyatuu, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Maandalizi yote ya Tamasha kubwa la Burudani lililopewa jina la DAR SUNSET CARNIVAL Coco Beach yamekamilika ambapo amewakaribisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye tukio Hilo la Aina yake.

RC Makalla amesema Tamasha hilo litatawaliwa na Burudani za aina mbalimbali ikiwemo Mziki mzuri kutoka kwa Wasanii akiwemo Barnaba, Sholo Mwamba, Gnako, Snura, Christina Bella, Kinata Mc, Mr Blue, Belle9 na wengineo na kutakuwa na Michezo ya watoto na Michezo ya fukwe.

Akizungumza wakati wa kikao kazi na Viongozi wa Wilaya, RC Makalla amesema dhamira ya Serikali ya Mkoa huo ni kuboresha fukwe ili ziwe sehemu Bora na rafiki kwa utalii.

Tayari mandhari ya ufukwe huo imeboreshwa na Wadau wa kampuni zote za Vinywaji zimekamilisha Ujenzi wa Vibanda vya kisasa ili kuhakikisha watu wote wanaofika kupumzika wanafurahia mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here