Home LOCAL PROFESA MBARAWA ATAKA KASI KUBWA SEKTA YA UJENZI.

PROFESA MBARAWA ATAKA KASI KUBWA SEKTA YA UJENZI.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akifungua mkutano wa pili wa wabunifu wa majengo na wakadiriaji Majenzi unaoendelea mkoani Arusha

Msajili wa Bodi ya wabunifu wa Majengo na wakadiriaji Majenzi akiongea katika mkutano wao unaoendelea mkoani Arusha

Na: Namnyaki Kivuyo.
Waziri wa ujenzi na uchuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa nchi imepiga hatua kubwa za maendeleo hivyo anatarajia kuwepo kwa kasi kubwa ya maendeleo  katika sekta ya ujenzi kupitia miradi ya serikali na sekta binafsi.

Profesa Mbarawa aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa pili wa wabunufu majengo na wakadiria majenzi(AQRB) ambapo alisema kuwa ni vema waendelee kusisitiza wataalamu kuwa na weledi wa kutosha katika kutoa huduma na kuweza kushindana na soko la Africa na Duniani kote.

Alisema anahamasisha wataalamu kuwezeshwa kujenga uwezo wa kiushindani kupitia miradi mbalimbali inayoendelea hapa nchini ambapo serikali kupitia wizara ya uchukizi ina mikakati ya kuwajengea uwezo wataalamu wake kwa kuwashirikisha kwenye miradi mikubwa.

Alisema taasisi zenye mamlaka kama AQRB,CRB,ERB na nyinginezo zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba wataalamu wanaopewa dhamana ya kutekeleza miradi wanazingatia sheria katika upatikanaji na uendeshaji wa miradi ya ujenzi kwani katika baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na wataalamu wa ndani utendaji wa kazi umesababisha malalamiko dhidi ya umahiri na ujuzi wa kampuni za ndani.

“Kaguzi ambazo zimekuwa zikifanywa na mamlaka ya usimamizi kwenye miradi yetu zimebaini mapungufu makubwa katika ubora wa kazi na gharama kubwa za miradi ndio mana nimefurahi kuwa katika mkutano huu ipo mada ya wajibu wa mamlaka za serikali kuwezeshwa wabunufu majengo, wakadiriaji majengo na wataalamu wanaoshabihiana katika kusimamia miradi kulingana na maadili ya kazi zao,”Alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake Rais wa wabunufu Majenzi (ACTET) David Kibebe alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kazi kutolewa bila ushindani huku sekta binafsi ikiwekwa kando ambapo miradi michache ambayo sekata binafsi imekuwa ikishirikishwa ni Ile ambayo fedha zinatoka benki ya dunia .

“Madhara ambayo yameshaonekana hadi sasa ni pamoja na wanafunzi waliopo vyuoni kukosa mahali pakufanyia mafunzo kwa vitendo kwani sio wote wanapewa nafasi katika taasisi za serikali, nyingine ni makampuni binafsi kushindwa kulipa kodi hali inayosababisha kufungwa kwa makampuni na vijana kukosa ajira,”Alisema Kibebe.

Alifafanua kuwa changamoto nyingine ni matumizi ya force akaunti ambapo kazi nyingi zimekuwa zikifanywa kwa kuangalia unafuu madukani na sio ubora wa vifaa katika kuhakikisha majengo yanadumu bila kuwa na misukosuko ya kuharibika mara kwa mara na kusababisha gharama kubwa za uendeshaji.

Naye Msajili wa bodi ya wabunufu majengo na wakadiriaji Majenzi Edwin Mnunduma alisema kuwa uchaguzi wa mada zitakazojadiwa katika mkutano huo umefanya mahususi ili kukumbusha wataalamu umuhimu wa kufuata na kuzingatia maadili ya utawala bora katika utekelezaji wa majukumu yao.

Alisema Hadi kufikia Septemba 2021 bodi imesajili wataalamu 1188 na kuwafuta 132 pamoja na kusajili makampuni ya kitaalamu 412 na kutafuta makampuni 72.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here