Home LOCAL OCEAN ROAD YAPOKEA MSAADA WA VITANDA VINAVYOTUMIA UMEME.

OCEAN ROAD YAPOKEA MSAADA WA VITANDA VINAVYOTUMIA UMEME.


DAR ES SALAAM.
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ya jijini Dar es Salaam imepokea msaada wa vitanda viwili (2) vya umeme kutoka nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Czech wakishirikiana na kampuni ya Gama Pharmaceutical kwaajili ya kumsaidia mgonjwa na muuguzi bila kutumia nguvu.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani (ORCI), Dkt.Julius Mwaiselage jijini Dar es Salaam leo Oktoba 07, 2021 amesema kuwa msaada walioutoa Serikali ya jamuhuri ya Czech ni dola 8000 ambazio ni sawa na shilingi milioni 18.

Dkt. Mwaiselage amesema kuwa mahitaji ya taasisi hiyo ni vitanda 25 vinavyotumi umeme au vya kieletrniki, vilivyokuwepo ni 8 sasa huku bado kuna mahitaji ya vitanda vingine 17 ili kutimia 25.

“Mahitaji ya vitanda hivi vinavyotumia umeme ni 25 sasa tuanavyo 8 tunahitaji vitanda vingine 17 vinavyotumia umeme, vitanda vingine vipo lakini sio vya umeme.” Amesema Dkt. Mwaiselage

Hata hivyo Dkt. Mwaiselage ameiomba kampuni ya kitanzania ya Gama Pharmaceutical iliyoshirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Czech kusaidia kupata vitanda vingine 17 ili kuendelea kutoa huduma inastahili kwa wagonjwa hospitalini hapo.

Amesema kuwa vitanda hivyo vinahitajika Zaidi katika hospitali hiyo kwani wagonjwa wa Saratani wameongezeka nchini kwa asilimia 60 hadi 70 wanaenda hospitali wakiwa na hali mbaya hadi hawawezi kutembea, hivyo vitanda hivyo vinaweza kufanya kazi nyingi vyenyewe vitakuwa ni mhimu zaidi.

Dkt.Mwaiselage amesema kuwa vitanda hivyo vitatumia umeme kwaajili ya kumpandisha mgonjwa juu au chini, vinabinuka kulingana na inavyotakiwa na Muuguzi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Omary Ubuguyu amesema kuwa vitanda vinavyotumia umeme vinahitajika Zaidi katika hospitali zinazotoa huduma ya dharura, sehemu ambazo zinatolewa huduma za wagonjwa mahututi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here