Wachezaji wa timu ya mpira wa Pete wa Wizara ya Nishati wakiwa tayari kwa Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Taasisi na Idara za Serikali (SHIMIWI) katika hatua za Makundi dhidi ya Tume ya Walimu, Octoba 21, 2021 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Wachezaji wa timu ya mpira wa Pete wa Wizara ya Nishati( wenye sare ya Bluu) wakicheza Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Taasisi na Idara za Serikali (SHIMIWI) katika hatua za Makundi dhidi ya Tume ya Walimu, Octoba 21, 2021 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Na: Zuena Msuya Morogoro.
Timu ya Mpira wa Pete ya Wizara ya Nishati imeiubuka mshindi dhidi ya Tume ya Walimu kwa kuwafunga magoli 14 kwa 5, katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Taasisi na Idara za Serikali (SHIMIWI) katika hatua za Makundi.
Mchezo huo ulichezwa dakika 40 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro, Octoba 21, 2021, ambapo kipindi cha kwanza kwa ya mapumziko Nishati waliongoza kwa magoli Tisa wakati Tume ya Walimu wakiwa na magoli 3.
Akizungumzia mchezo huo, Nahodha wa Timu ya Nishati, Fortunata Getele alieleza kuwa kipindi cha pili cha mchezo huo Nishati ilijiongezea ushindi zaidi kwa kuongeza magoli mengine 5, na Tume ya Walimu magoli 2, na kuipa ushindi Nishati kwa Magoli 14 dhidi ya Tume ya Walimu iliyoambulia magoli 5 tu katika kipindi chote cha mchezo.
Katika hatua za makundi katika mashindano ya SHIMIWI, Wizara ya Nishati imepangwa katika kundi “A” ikicheza na Timu ya Wizara ya Sanaa, Tamaduni na Michezo, Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi(OSHA), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, pamoja na Tume ya Walimu.
Michezo hiyo bado inaendelea hadi Novemba 2, 2021.