Home SPORTS MKETO: SIMBA TUNAIMALIZA KESHO

MKETO: SIMBA TUNAIMALIZA KESHO

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

VINARA  wa ligi kuu Tanzania bara Polisi Tanzania wamesema kuwa kikosi kimejipanga vyema  katika mchezo wao  dhidi ya  Simba utakaopigwa katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari kocha msaidizi Geogre Mketo amesema kuwa anatambua kikosi cha Simba ni kipana hivyo amejipanga kucheza vyema na kupata matokeo.

“Sina shaka na kikosi changu kwani kimejipanga vyema kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo huo ambao lengo letu ni kufanya vyema katika mchezo huo ambao tunajua Simba wametoka kupoteza katika michuano ya kimataifa  hilo sisi tunalifaham na tumejipanga kuhakiksha tunaongeza maumivu huu yao.

Amesema kuwa kikosi kipo imara katika mtanange huo kwani wanatambua ukubwa wa bingwa mtetezi Simba ambaye kwa sasa ana jumla ya pointi 4 huku polisi ikiwa na pointi 9.

Kwa upande na Nahodha wa timu ya polisi Tanzania Juma Ramadhani  alisema Kuwa kesho ni siku ya kuvunja miiko kwa kuifunga Simba.

“Tunajua polisi imekuwa na matokeo mabaya kwa simba lakini kwa kesho lazima simba ifungwe ili kuendelea kukaa kileleni cha ligi kuu Tanzania bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here