Home LOCAL MEYA KUMBILAMOTO AWATAKA MADIWANI WENYEVITI ILALA KUACHA NONGWA

MEYA KUMBILAMOTO AWATAKA MADIWANI WENYEVITI ILALA KUACHA NONGWA

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto akimkabidhi CERTFICATE of Appreciation Mwenyekiti wa Mtaa wa Amani Kata Kipunguni DANI MALAGASHIMBA CERTFICATE hiyo aliyekabidhiwa MALAGASHIMBA imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam kwa kumuunga mkono juhudi zake za kuisaidia Serikali (katikati)DIWANI wa Kipunguni Steven Mushi( PICHA NA HERI SHAABAN).

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Amani Kata Kipunguni wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya Serikali za Mtaa ambayo imejengwa na Mwenyekiti (kushoto )Diwani wa Kipunguni Steven Mushi (PICHA NA HERI SHAABAN).

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya JijiTabu Shaibu akizungumza leo wakati wa Ufunguzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Amani Kata Kipunguni (kushoto)Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto (PICHA NA HERI SHAABAN).

NA: HERI SHAABAN.

MEYA wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amewataka Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Wilaya ya Ilala kuacha nongwa na Malumbano  katika Kata  zao badala yake wafanye Kazi za kuwatumikia wananchi na kusimamia miradi ya Maendeleo.

MEYA Kumbilambito aliyasema hayo Kata ya Kipunguni Wilaya ya Ilala wakati wa kufungua ofisi ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Amani iliyojengwa kwa fedha za Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa DANIEL MALAGASHIMBA sio Fedha ya Serikali.

“Madiwani wangu wa Wilaya ya Ilala na Wenyeviti wote naomba mshirikiane kutatua kero za wananchi mumsaidie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassani Suluhu mtatue kero na kusimamia miradi ya Maendeleo muache nongwa Wananchi wanataka Maendeleo”alisema Kumbilamoto

Kumbilamoto alisema baadhi ya Madiwani kwenye Kata wanashindwa kusimamia miradi ya Maendeleo  na kubuni miradi mipya wanagombana na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa huku wakikwamisha Maendeleo.

Alimtaka Diwani wa Kipunguni Steven Mushi ashirikiane na Mwenyekiti wake wa Serikali za Mtaa DANIEL MALAGASHIMBA waondoe tofauti zao kwa sasa watumikie wananchi wanaowaongoza ili kuleta Maendeleo kusimamia miradi kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassani Suluhu, kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda.

Alimpongeza Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa DANIEL MALAGASHIMBA  kwa kujenga ofisi ya Afisa Mtendaji wa Mtaa ya Kisasa kwa Fedha zake pamoja na wadau wa Maendeleo waliomsaidia akiwemo Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe aliyechangia mabati kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo 

Kumbilamoto aliwataka wamuogope Mwenyezi Mungu badala yake watekeleze Ilani ya chama cha Mapinduzi.

MEYA Kumbilamoto katika kuunga mkono juhudi za MALAGASHIMBA alisema atatoa msaada wa TV kwa ajili ya ofisi wawe wanafatilia Taarifa za habari na kumuunga mkono Rais Samia Hassan Suluhu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Amani  DANIEL MALAGASHIMBA alisema Mtaa huo ulizaliwa 2017 baada kugawanywa kwa uliokuwa Mtaa Mama wa  kipunguni na kupelekea kupatikana kwa mitaa minne yaani Machimbo,Kitinye,Kipunguni na Amani.

MALAGASHIMBA alisema awali waliweka Ofisi kwa wananchi wakifadhiliwa ambapo kwa sasa amemshukuru mdau wa Maendeleo Dankan Mwaisumo aliyejitolea kiwanja kwa ajili ya Ofisi ya Mtaa wa Amani na Huduma za jamii katika kunga mkono juhudi za Mwenyekiti  wa Amani.

MALAGASHIMBA alielezea gharama za ujenzi wa ofisi hiyo alisema jumla ya shilingi Milioni 10 ndio zimejenga jengo hilo la kisasa  Fedha zake binasfi bila fungu la Serikali alishirikiana na wadau wa Maendeleo.

Akielezea changamoto za Mtaa wa Amani choo cha Ofisi ya Serikali za Mtaa amna ,changamoto zingine Barabara mbovu Moshi Baa kwa Mkolemba hali inayopelekea wanaotumia vyombo vya usafiri kupandisha gharama za Daladala kufika eneo hilo kutoka 400 hadi 700.

MALAGASHIMBA alisema changamoto nyingine Soko na Kituo cha Polisi amna kwa sasa ameiomba Serikali ya kuzitatua changamoto hizo wananchi wafurahie matunda ya Serikali yao.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji TABU SHAIBU alimkabidhi MALAGASHIMBA CERTFICATE OF APPRECIOATION  iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jumanne Shauri kwa juhudi zake nzuri kuisaidia Serikali .

Kaimu Mkurugenzi Tabu Shaibu alisema juhudi za MALAGASHIMBA ni Mfano wa kuigwa ndani ya Wilaya ya Ilala Mwenyekiti wa Mtaa amefanya mambo makubwa kujitolea kwa gharama zake ujenzi wa ofisi bila kushirikisha Serikali.

“Halmashauri imechukua changamoto ya choo cha Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Amani mpaka mwezi Desemba choo kitakuwa kimekamilika ili kiweze kutumika ” alisema Tabu .

Mwisho

Previous articleYANGA, AZAM NANI MBABE LEO.
Next articleRAIS SAMIA SULUHU HASSAN AONDOKA NCHINI KWENDA GLASGOW SCOTLAND
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here