NA: HERI SHAABAN.
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salam Omary Kumbilamoto amewataka wazazi wa Wilaya ya Ilala kuwekeza sekta ya elimu kwa watoto wao wazingatie elimu.
Meya Kumbilamoto aliyasema hayo katika mahafali ya kwanza darasa la saba ya Mtakatifu St ,JB ‘Cottolengo iliyopo Kata ya Vingunguti wilayani Ilala.
“Nawaomba wazazi wangu wa halmashauri ya jiji la Dar es salaam tuzingatie elimu kwa kuwekeza sekta ya elimu kwa watoto wetu ili wasome kwa bidii kukuza taaluma” aĺisema Kumbilamoto.
Alisema wazazi wakiwekeza sekta ya elimu Taifa letu litapata wanasayansi,,Madaktari na watalaam mbalimbali kwa ajili ya kujenga nchi yetu .
Aidha Meya aliwataka wazazi kujenga tabia ya kukagua daftari za watoto wao pindi wanaporudi shule .
Aidha pia aliwataka wazazi wa wilaya ya Ilala kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kila jambo.
Wakati huohuo Meya alitoa ahadi ya kusaidia vitabu vya shule vyenye thamani ya shilingi 600,000/=
Kwa ajili ya shule hiyo ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania.
Meya Kumbilamoto aliagiza uongozi wa Shule ya Mtakatifu st,JB COTTOLENGO kuanza mikakati ya kuanda kidato cha kwanza mwakani Wanafunzi wasome hapo wazazi wasipeleke watoto mbali .
Meya alisema atafanya mchakato wa kuwatafutia eneo kwa ajili ya upanuzi wa Shule hiyo.