MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, amesema kata ya Segerea Wilayani Ilala inatarajia kuwa ya Kisasa kwa kujenga miundombinu ya Barabara na Kituo cha afya cha kisasa Segerea .
Mbunge Bonah aliyasema hayo leo katika ziara yake kata ya Segerea kuangalia miundombinu ya barabara na vikao vya wananchi vya kutatua kero .
“Kata ya Segerea ambayo imebeba jina la Jimbo la Segerea lazima iwe ya kisasa Serikali imetoa pesa kwa ajili ya upanuzi wa zahanati Ugombolwa kutoka zahanati inapanuliwa na kuwa kituo cha afya kikubwa ndani ya Jimbo la Segere na mchakato wake wa ujenzi umeanza” alisema Bonah.
Alisema serikali wanajenga hospitali kubwa ya Serikali ili wananchi wapate huduma karibu.
Pia Mbunge Bonah alisema baadhi ya Barabara za kata ya Segerea barabara zitajengwa na Mradi wa UNDP na zingine zitakuwa chini ya usimizi wa TARURA ikiwemo kalavati za segerea na machimbo na Ugombolwa.
Amewawata wakazi wa Kata ya Segerea walioziba hifadhi ya barabara kuacha maeneo hayo wazi ili wasikwamishe mradi barabara zikijengwa thamani itapanda Segerea na fursa zitaongezeka.
Kwa upande wake Diwani wa Segerea Robart Manangwa alisema Kituo cha afya kitakachojengwa Segerea kitakuwa na jengo la upasuaji ,jengo la huduma ya mama na Mtoto,jengo la kulaza wagonjwa na chumba cha kuifadhi maiti (Mochwali)na Xray .
Aidha Diwani Robart alisema mikakati yake kipaumbele kujenga barabara nane ukubwa wa KM 9 baadhi ya barabara hizo Stakishari Oil Com,Mila Colo Hospitali ,Chang’mbe Segerea Zahanati na Segerea Kusini.
Mwisho