MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, amepokea kero za wananchi Kisukuru kuhusu mikopo ya serikali.
Mbunge Bonah alipokea malalamiko hayo katika ziara yake kata ya Kisukuru Dar es Salam jana ambapo wakazi wa kata hiyo walisimama wakilalamikia mikopo inayotolewa ngazi ya halmashauri ya Wanawake Vijana na Watu Wenye Ulemavu wakidai aijawafikia walengwa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mbunge Bonah alisema kuhusu suala la mikopo ya halmashauri Diwani wa Kisukuru Lucy Lugome atafatilia na kusimamia vikundi vyote vya kata hiyo vitaweweshwa.
Katika hatua nyingine Bonah aliwaeleza suala la upanuzi wa barabara ambapo alisema mradi wa barabara hauna fidia barabara za kisasa zitajengwa Maji chumvi kwenda Extenal mradi unafadhiliwa na Benki ya Dunia .
Aidha Mbunge alisema Kata Kisukuru inatarajia kuwa ya Kisasa barabara zitajengwa sambamba na mifereji itapita katika makazi ya watu hivyo lazima vikao vya wananchi vifanyike kwa sababu miradi mingi inakuja aina fidia.
Akizungumzia Maendeleo alisema ujenzi wa Zahanati ya Kata mradi ulishindwa kujengwa baada kiwanja kuuzwa pesa ya ujenzi wake kukaa benki muda mrefu.
“Kata ya Kisukuru imekuwa na changamoto Ujenzi wa kituo cha polisi pia ilikuwa changamoto pesa yake ilikaa benki zaidi ya miaka mitano mradi ukachelewa kuanza kwa wakati” alisema Bonah.
Diwani wa Kata ya Kisukuru Lucy Lugome alisema suala la mikopo ya vikundi ambayo inatolewa ngazi ya halmashauri kwa vikundi amewataka wasimbebeshe mzigo Mbunge yeye Diwani wa kata hiyo atashughulikia.
Diwani Lucy alisema mikopo ya vikundi ya Wanawake vijana na watu wenye ulemavu atafatilia na kuwakikisha wananchi wake wanapata fursa hiyo na kujikwamua kiuchumi .
Ziara hiyo pia ilikagua miradi ya maendeleo ya kata ya Kisukuru ,ikiwemo sekta ya elimu na Kituo cha Polisi cha Kisasa.
Mwisho.