Home SPORTS MASHABIKI 10000 KUIONA STARS KWA MKAPA

MASHABIKI 10000 KUIONA STARS KWA MKAPA

 

 

Na:Stella kessy, DAR ES SALAAM.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeruhusu mchezo baina ya Taifa Stars na Benin kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuingia mashabiki wasiozidi 10,000

Kauli hiyo imetolewa na ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa wamepokea taarifa hiyo kutoka CAF wakiruhusiwa kuingiza namba hiyo ya mashabiki katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia

“Tumepata taarifa hii kwa kuchelewa lakini sio sababu ya mashabiki kushindwa kuja kuisapoti timu yao. Watu 10,000 ni wengi lakini kulingana na ukubwa wa Uwanja wa Mkapa ni wachache hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi,” amesema Ndimbo

Awali taarifa zilidai kuwa mashabiki hawatoruhusiwa kuingia uwanjani katika mechi hiyo na hiyo ilitokana na kuchelewa kwa CAF kurudisha majibu ya ombi la TFF la kuruhusiwa kuingiza mashabiki

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here