Mwandishi wetu, Dodoma.
Uchaguzi wa Viongozi wa Chama Mchezo wa Netiboli Tanzania (CHANETA) umekamilika na viongozi wa kukisimamia chama kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa Katiba inavyotaka.
Uchaguzi huo umefanyika jana katika ukumbi wa hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo kukamilika Mwenyekiti wa uchaguzi kutoka BMT Milinde Mahona amewataka viongozi hao wapya wa chaneta kuhakikisha wanasimamia Katiba ya chama na Sheria ya BMT katika kutekeleza majukumu yao.
Viongozi waliopatikana katika uchaguzi huo kwa nafasi ya Mwenyekiti ni Dkt. Devotha Marwa ambaye ametetea nafasi yake kwa kupata kura 27 za ndiyo kati ya mpinzani wake Dkt. Juliana Manyerere aliyeibuka na kura 05.
Nafasi nyingine niya Katibu Msaidizi iliyochukuliwa na Hilder Mwakatobe aliyeibuka na kura 24 dhidi ya mpinzani wake Sophia Nchimbi mwenye kura 06, nafasi nyingine niya Mweka hazina mgombea pekee Mary Chalamila aliyeibuka na kura 27 kati kura halali 38.
Naye Mwenyekiti wa Chama Dkt.Devotha Marwa akiwataka viongozi wenzake kuimarisha ushikiano na hasa viongozi wa Mikoa ambayo ndiyo wanachama wao.
Katika uchaguzi huo nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu zimebaki wazi kwakuwa wagombea hawakukidhi vigezo ambapo nafasi hizo zitajazwa katika uchaguzi mdogo hapo baadae.