KIKOSI cha Yanga kesho kinatarajia kuondoka kuelekea Arusha kwa ajili ya kuweka kambi katika kipindi cha mapumziko.
Hata hivyo kikosi hicho inaondoka na jumla ya wachezaji 22 ambao hawajaitwa katika timu ya taifa.
Kauli hiyo aliitoa baada ya kumaliza mechi yao dhidi ya Geita Gold kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema timu hiyo itaweka kambi Arusha katika muda wa mapumziko kupisha kalenda ya mechi za Fifa.
Nabi amesema muda huo atautumia kurekebisha makosa aliyoyaona katika michezo iliyocheza hivi karibuni.
“Natambua timu yangu bado haijawa sawa ila nimefurahia ushindi ambao nimepata tangu kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara hata hivyo kwa muda ambao ligi imesimama na nitapisha kalenda ya Fifa timu yangu haitapumzika bali tutaelekea Arusha kuendelea na maandalizi ya mechi zijazo” amesema kocha Nabi.
Yanga imeshinda mechi zake zote mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo mechi ya kwanza ya Yanga ilibahatika kuchukua ngao ya jamii pamoja na kushinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na walishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold.