Home SPORTS KIBU AAHIDI MAKUBWA SIMBA.

KIBU AAHIDI MAKUBWA SIMBA.


Mwandishi wetu.

BAADA ya suala la vibali kutoka serikalini kukamilika Mshambuliaji Kibu Denis amehaidi kujitoa hadi jasho la mwisho kuhakikisha simba inapata mafanikio

Kibu amesema baada ya klabu kumuamini na kimsajili anajikuta  ana deni kubwa na kuahidi kulipa kwa kuisaidia  timu uwanjani kila atakapopata nafasi.

Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa simba ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri hivyo ili kupata  nafasi ya kucheza  unapaswa kujituma kulishawishi benchi la ufundi.

“Wanasimba wasubiri tu mambo mazuri yanakuja wameonyesha imani kubwa kwangu nami nitawalipa uwanjani hiyo ndio ahadi yangu kwako “amesema.

 Hata hivyo kwa sasa kibu yupo nchini Benin na kikosi  cha timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) kinachoshuka kesho katika mchezo wa marudiano dhidi ya Benin.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here