Home LOCAL KATIBU MKUU UVCCM TAIFA: RAIS SAMIA ANAWAPENDA NA KUWAAMINI VIJANA.

KATIBU MKUU UVCCM TAIFA: RAIS SAMIA ANAWAPENDA NA KUWAAMINI VIJANA.



Ni katibu mkuu UVCCM taifa Kenan Kihongosi akiongea na vijana Arusha baada ya kuzindua UVCCM jogging club Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akiongea na vijana kuhusiana na ujio wa Rais mkoani Arusha baada ya uzinduzi wa UVCCM jogging club Arusha.
Ni mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima akiongea na vijana baada ya uzinduzi wa UVCCM jogging club Arusha.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Katibu mkuu wa ummoja wa vijana  wa chama  mapinduzi taifa (UVCCM)Kenan Laban Kihongosi amesema kuwa Rais wa Jamuhuri ya muunganao wa Tanzania Samia Hassan Suluhu anawapenda na kuwaamini vijana kwani vijana ndio nguvu kazi ya taifa.

Kenan aliyasema hayo wakati akizindua UVCCM jogging club Arusha ambapo 

Amempongeza mkuu wa mkoa kwa namna anavyoongoza mkoa was Arusha ambapo alisema kuwa Rais Samia anawapenda vijana na anajua jinsi wanavyofanya kazi kwa weledi ndio amewapa nafasi mbalimbali za uongozi.

“Uwepo wa vijana katika nafasi mbalimbali za uongozi ni ishara moja wapo kuwa Rais wetu anatupenda na kutuamini vijana na leo anaingia Arusha tunataka ajue kuwa Arusha kuna vijana waliopo nyuma yake tujitokeze kwa wingi kwenda kumlaki lakini pia kesho tujae kwenye uwanja huu kwani vijana peke yetu tunaweza,”Alisema Kenan.

Alifafanua kuwa Rais Samia ni mtu anayejali shida za watanzania ndi Mana juzi Dododo  alitoa fedha kwaajili ya shule mbalimbali katika halmashauri ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya afya kwa kununua vifaa mbalimbali ambavyo havikuwepo katika hosipitali za taifa, kanda, mikoa na wilaya.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela  aliiunga mkono uzinduzi wa jogging na kusema kuwa ni sehemu ya kuwaweka vijana pamoja kwaajili ya umoja wao lakini pia ni sehemu ya kuboresha afya zao lakini  kwa kuwa wanakazi ya kumpokea Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kesho baada ya kutoka kanisani waje waungane washikaman.

Naye meya wa jiji la Arusha MaxMillan Iranqe alisema kuwa ananawaamini vijana wa Arusha kuwa  kesho watajitokeza kwa wingi tumpokee Rais  ikiwa ni sehemu ya kumshukru kwa mengi aliyoyafanya mojawapo ikiwa ni  kufanya mchakato ulioweza kuwaleta watalii  tena.

 “Kesho jiji la Arusha Rais atamimina  bilioni 1.3  kwa wanawake vijana na wenye  ulemavu tunataka kila kijana afanye kazi atoke kwenye hali ya chini na kuacha kuwa tegemezi na hili litawezekana mkipata mkopo kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali njooni na Kama mtu kesho atakuwepo Kati ya watakaopokea fedha hizi msikate tamaa awamu nyingine unakuja tutamfikia kila kijana mwenye uhitaji,” Alisema  Meya jiji la Arusha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here