Home BUSINESS KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA VILAINISHI VYAKE VIPYA, (PUMA LUBRICANTS)

KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA VILAINISHI VYAKE VIPYA, (PUMA LUBRICANTS)

Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah (kulia) pamoja na Meneja wa Oil na Vilainishi wa Puma Energy Prosper Kasenegala (kushoto) wakikata utepe kuzindua bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy kwenye hafla fupi ya uzinduzi huo hafla Jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) wakizindua Bidhaa za vilainishi vinavyomilikiwa na Puma.


Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy wa Afrika Bw.Fadi Mitri akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Bw.Dominic Dhanah akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited inayoongoza kwa uzalishaji wa Mafuta nchini Tanzania imeanzisha laini yake mpya ya Vilainishi kwenye soko nchini “Puma Lubricants” vyenye kukidhi mahitaji yote ya Magari, Viwanda na Mitambo mbalimbali. Hatua hii inafuatia nia ya dhati ya kampuni ya Puma Energy ya Kuhamasisha Mabadiliko ya tabia “inspiring change” na lengo letu ni kuhamasisha wateja wetu na watu wengine kugundua chaguzi mpya na kufanya mambo kitofauti na kwa ubora Zaidi.

Akiongea na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma Energy Bwana Dominic Dhanah amesema uwa mara zote wamekuwa wakiumiza vichwa kutafuta namna bora zaidi ya kuboresha bidhaa na huduma wanazozitoa.

“Ndugu zangu watanzania, hatulali, kila siku tunafikiria na kuumiza kichwa kutafuta namna bora zaidi ya kuboresha bidhaa na huduma zetu. Leo hii tumewaletea vilainishi vya Puma. Vilainishi hivi sio tu ni bora sana na vya hali ya juu lakini pia ni utaratibu wa kisasa wa kuchochea tabia mpya ya kuchagua kilicho bora zaidi” Amesema na kuongeza kuwa vilainishi hivyo vimetengenezwa na kuratibiwa nchini Uswisi kwa kuzingatia matakwa na ubora wa viwango vya kidunia na nchini kwa ujumla. 

Kwa upande wake Bw. Fadi Mitri Mkuu wa kampuni ya Puma Energy wa Afrika aliongeza, “Puma Energy itawekeza Zaidi ya dola milioni 100 (takribani Bilioni 230) katika miaka 3 ijayo nchini Tanzania, uwekezaji huu nia katika mwenendo wa jitihada za kampuni kuifikia jamii na Aliongeza pia “Tungependa kualika wateja wetu wanaothaminiwa sana” Kubadilisha machaguo yao na kuchagua Oil na vilainishi chapa Puma Energy kwani ni aina mpya ya vilainishi vinavyo kuhakikishia ulinzi bora wa injini yako, vifungashio vya kibunifu, na taknolojia ya hali ya juu ambayo tutengenezwa kwa mafuta ya hali ya juu na yenye viwango vya chini vya Sulphur na faharisi ya mnato mwingi. (high viscosity)”.

Kwa upande wake Bwana Prosper Kasenegala, Meneja wa Oil na vilainishi wa Puma Energy aliwasihi watanzania wotwe watumie vilainishi vya Puma; na kusisitiza kuwa Oil na vilainishi hivyo vya Puma Energy sasa yanapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya Puma Energy nchini kote na kwamba ni kipaumbele cha kampuni ya Puma Energy kuhakikisha vilainishi vyenye ubora vinapatikaa kwa wateja wetu muda wote.


Meneja wa Oil na Vilainishi wa Puma Energy Bw.Prosper Kasenegala akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya vilainishi vinavyomilikiwa na Puma Energy ambapo hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 


Meneja Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited Venessy Chilambo akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla hiyo kuelezea bidhaa hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here