MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wameibuka na ushindi 1-0 dhidi ya Dodoma jiji katika mchezo uliopigwa dimba la Jamhuli.
Kikosi hicho kimepata ushindi kupitia nyota wao Meddie Kagere ambaye alianzia benchi amepachika bao hilo dakika ya 69 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 na lilimshinda kipa wa Dodoma Jiji Hussein Masalanga na kuifanya Simba kusepa na pointi tatu.
Simba kwa sasa wamefikisha pointi nne na kuwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza baada ya kucheza mechi mbili.
Dodoma Jiji walikamilisha dakika 90 wakiwa pungufu kwa kuwa nyota wao Anuary Jabir alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonekana akimchezea faulo Kenned Juma ambaye hakumaliza dakika 90.
Kwa upande wa Mkuu wa kikosi cha Dodoma jiji, Bwana Makata amesema kuwa kadi nyekundu aliyopewa Anuary Jabir katika dakika ya 44 imesababisha kikosi kishindwa kupata matokeo.
Anasema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na wachezaji walipambana kupata matokeo.
“Mimi sina shaka na kikosi changu japo tumepoteza mchezo wa leo lakini tunajipanga kwa michezo ijayo” anasema.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa Simba Seleman mayola Matola anasema kuwa katika mchezo wao leo ulikuwa kama vita sababu ya mpira ulikuwa na ushindani sana.
Anasema kuwa mchezo ulikuwa mgumu wachezaji wamejituma kupata matokeo ambayo yanaweka kikosi katika hali ya morali.