Home LOCAL IDARA YA ELIMU HALMASHAURI YA JIJI YAPOKE MADAWATI

IDARA YA ELIMU HALMASHAURI YA JIJI YAPOKE MADAWATI


NA: HERI  SHABAN.
IDARA ya Elimu Msingi Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imepokea msaada wa madawati 100 kwa ajil i ya Shule ya Msingi Kisutu  wilayani Ilala

Msaada huo umetolewa na wadau wa sekta ya elimu Benki ya Canara Tanzania kwa ajili ya kuunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Mungano Tanzania ya Rais Samia Hassan Suluhu .

Afisa Elimu Msingi Sipora Tenga ameshukuru Benki ya Canali kwa juhudi zao za kuisaidia Serikali amewataka wadau wengine kuunga mkono serikali.


“Halmashauri ya Dar es Salaam ina Shule 121 kata 36 katika zangu zimekuwa zikifanya vizuri mwaka hadi mwaka katika ufaulu kutokana na mazingira mazuri ya shule na taaluma”alisema Sipora.

Afisa Elimu Sipora alisema Wilaya ilala ina wanafunzi wengi amewataka wadau kuunga mkono katika sekta ya elimu ili Taifa letu lipate wasomi bora na viongozi wa baadae.


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kisutu Elizabeth Masawe, alisema awali shule hiyo ilikuwa ya kidini kwa madhehebu ya Wahindi mwaka 1971 Serikali ilichukua shule hiyo kuwa ya serikali hadi sasa ina wanafunzi jumla 1693.

Mwalimu Masawe alisema kati ya wanafunzi 1693 wavulana 751 wasichana 942 walimu 23 wakike 22 wakiume mmoja .

Afisa oparesheni wa Benki ya Canara Tanzania John Charles alisema wao kama Benki wanaunga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili watoto waweze kusoma.

Mwisho.

Previous articleMAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AIAGIZA SHIRIKA LA POSTA KUTUMIA FURSA YA BIASHARA KATIKA UKANDA WA SADC
Next articleTANZANITE YAICHAPA ERITREA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here