Home SPORTS GOMES OUT SIMBA, HITIMANA ACHUKUA MIKOBA YAKE

GOMES OUT SIMBA, HITIMANA ACHUKUA MIKOBA YAKE

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KLABU ya Simba imeridhia ombi la aliyekuwa kocha mkuu, Didier Gomes da Rosa la kuachana na  Simba kuanzia leo Septemba 26.

Baada ya tathimini na majadiliano ya kina pande zote zimefikiana kwa mujibu wa mkataba na manufaa ya wote.

Kutokana na hatua hiyo aliyekuwa kocha msaidizi Thierry Hitimana ndie atakuwa kocha mkuu wa simba katika kipindi hiki cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola .

Aidha klabu hiyo pia imefanya mabadiliko  madogo katika benchi la ufundi kwa kisitisha mikataba ya aloyekuwa kocha wa makipa Milton Nienob na kocha wa viungo Adel Zrane.

Klabu ya simba inamshukuru kocha Gomes na wenzake kwa mafanikio waliyoyapata katika kipindi chote waliokuwa simba na kuwatakiwa kila kheri huko waendako.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here