Home LOCAL GAMBO AMVAA DKT PIMA,AMUOMBA RC ARUSHA AMSHAURI AWE MTULIVU.

GAMBO AMVAA DKT PIMA,AMUOMBA RC ARUSHA AMSHAURI AWE MTULIVU.



NA: NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.

Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo amemvaa mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima kutokana na madai ya kuwa hakutaka kumualika katika kilele cha maadhimisho ya utoaji mkopo mkopo wa asimia kumi kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu ambapo kutokana na hayo alimuomba mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amshauri mkurugenzi huyo kuwa mtulivu.

Gambo aliyasema hayo baada ya kufika katikatukio hilo bila mualiko na kupewa nafasi ya kuongea na wananchi wake ambapo alisema kuwa mbunge ni sauti ya watu,wananchi wakilia analia nao na wakicheka anacheka nao hivyo  mkurugenzi huyo asimpuuzie kwani akimpuuzia anakuwa amewapuuza wananchi.

Alieleza kuwa kuwa kama mbunge akikaa nyuma ya mgongo wa serikali anakosa sifa za kuwa mbunge kwani atashindwa kutekeleza wajibu wake wa kufikisha shida za wananchi serikalini lakini kuna watu hawalielewi hilo.

“Mkurugenzi alikataa kumualika hapa alafu anatoa sababu za uongo kuwa nipo kwenye vikao vingine namwambia tu asimchukulie mbunge kama mtu mwepesi kwani walipata kura kwa shida, jimbo la Arusha mjini sio jimbo rahisi, tulizuka kata zote 25 kuomba kura Jimbo lirudi CCM yeye alikuwa amekaa tu ofisini,” Alisema Gambo.

Aidha alimuomba Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela kumshauri mkurugenzi huyo kuwa mtulivu kwani hawezi kumkataa mwakilishi wa wananchi hivyo ashirikiane nae katika kufanya kazi.

“Kati yetu wote tuliopo hapa Mimi ndio nimechaguliwa kwa kura nyingi na wananchi, wameniamini na kuona nafaa kuwawakisha na wanaofuata kwa kuchaguliwa ni madiwani  ni tofauti na yeye aliyeteuliwa tuu, Alisema.

Sambamba na hayo pia Gambo alisema kuwa mtiririko wa kuwapanga machinga katika maeneo yaliyoainishwa yanahitaji uangalifu mkubwa na sio kuiachia halmashauri peke yake kwasababu wanapenda kukusanya ushuru kwani haoni jitihada za dhati za machinga kupewa vitambulisho.

“Nguvu inayotumika na jiji na TRA ni ndogo ni kama  hawawataki wala hawawahitaji machinga katika katika jiji letu kwahiyo naomba pia mkoa uliangalie hili,” alisema Gambo.

Kwa upande wake  Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela  katika aliwataka madiwani kukaa karibu na wananchi kwani kazi iliyofanyika jiji la Arusha ni kubwa  hivyo wakasimamie tija ya mikopo hiyo ili  vigezo vya makundi yote matatu yazingatiwe na kuweza kuwafikia wale watu wa chini kabisa ili iwasaidie  kuwajenga.

kwa upande wa Machinga mkuu wa mkoa alisema kuwa maelekezo ya Rais wameyaelewa hivyo asitokee mtu akapata vishashawishi kuwa anaweza kukwamisha mpango huo kwani hawatamuacha ambapo akisema watahakikisha machinga wanapata maeneo yenye staha na yatakayowajenga ambapo ameomba viongozi wote washitikiane katika hilo.

Aidha kuhusiana na tuhuma alizozitoa mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo dhidi ya mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima  mkuu wa mkoa aliwataka viongozi kushikamana kwani kupendana sio kudanganya a bali ni kuambiana ukweli mchana kweupe na mbunge anampenda mkurugenzi ndio mana amemuambia ukweli hadharani.

Naye mkurugenzi wa jiji la Arusha John Pima alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jiji linatarajia kukusanya zaidi ya billion 23 na kwa robo ya kwanza wanaotarajia kutoa mkopo wa shilingi billion 2.1 kwa makundi hayo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Tajieli Mahenga kaimu afisa maendeleo jiji la Arusha amesema wametenga Billioni 2,158,905,050.00 ambapo wametoa mkopo kwa vikundi vya wanawake 88 shilingi Bilioni 1,196,883,000.00, vikundi 51 vya vijana  shilingi  million 887,130,040.00 na vikundi 9 vya walemavu wamepewa shilingi million 74,892,010.00.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here