Mwandishi wetu.
WENYEKITI wa klabu kongwe hapa nchini, Murtaza Ally Mangungu wa Simba SC na Dk Mshindo Mbette Msolla wamejitokeza kuwania Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB).
Wawili hao ni kati ya wagombea watatu tu waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti pamoja ma Mwenyekiti wa sasa, Steven Jarvis Mnguto wa Coastal Union ya Tanga.
Uchaguzi wa TPLB umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao baada ya usaili utakaofanyika kati ya Novemba 26 na 28, mwaka huu.