Home SPORTS DEO LUCAS AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA MAZOEZINI.

DEO LUCAS AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA MAZOEZINI.

 

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KOCHA  msaidizi wa timu ya taifa  soka la ufukweni Deo Lucas amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika mazoezi ya timu ya hiyo   ambayo inajiandaa kwa ajili ya michuano ya COSAFA  yanayotarajiwa kutimua vumbi  Novemba 8 -14 huko Durban Afrika kusini.

Amesema kuwa kikosi kinaendelea kujifua kwa ajili ya kufanya vyema katika michuano hiyo huku lengo la timu ni kufanya vyema na kuitangaza nchi kwa kuibuka na ushindi.

“Kwasasa kikosi kipo katika mazoezi takribani wiki ya pili kikosi kikiwa ba ushindani ambapo wiki iliyoisha tuliandaa mechi ya kirafiki  dhidi ya kombaini ya vilabu ya soka  ilikuwa ni sehemu ya kucheki kikosi kwa wiki ya kwanza ambayo tumeanza mazoezi “alisema 

Aliongeza kuwa kuwanzia kesho wataanza mazoezi kwa siku mara mbili ili kuweka kikosi katika hali ya maandalizi ya kuibuka na ushindi katika michuano hiyo.

Amesema kuwa mpaka sasa kikosi kinaendelea vyema na mazoezi ya kujiandaa kwa ajili ya kupata ushindi katika michuano hiyo ambayo ipo mbele ya kikosi hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here