Home SPORTS BIASHARA UTD YAIPIGA AL AHLY TRIPOLI 2-0 KWA MKAPA

BIASHARA UTD YAIPIGA AL AHLY TRIPOLI 2-0 KWA MKAPA

 Na: Stella Journalist: Stella Kessy

BIASHARA  United leo imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya  ya Al Ahly Tripoli ya Libya katika
michuano ya kombe la shirikisho mchezo uliopigwa dimba la mkapa jijini Dar es Salaam.

Mtanange wa aina yake huku kikosi cha biashara kikiwa katika hali ya kutafuta ushindi na kupata bao   katika dakika ya 40   Deogratius  judica ameipatia timu yake bao  ambalo lilidumu Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Katika kipindi cha pili mchezaji  Atupele Green aliipatia timu yake bao la pili katika  dakika ya 61 bao ambalo lilidumu katika dakika 90.

Kocha Mkuu wa Biashara  Patrick  Okumu amesema kuwa kikosi chake kipo vizuri ndio maana amefanikiwa kupata matokeo.

Amesema kuwa anawaomba wadau  na watanzaia waendelee kuiombea timu yao pia kuwa  na imani na kikosi kitaenda kufanya vyema katika mchezo wa marudiano dhidi ya wapinzani wao.

Hata hivyo kikosi cha Azam kesho majira ya saa 9:00   watawaalika Pyramids ya Misri katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here