Home BUSINESS BENKI YA TCB YAIPONGEZA SERIKALI KUWEKA MIFUMO IMARA YA KIFEDHA NCHINI.

BENKI YA TCB YAIPONGEZA SERIKALI KUWEKA MIFUMO IMARA YA KIFEDHA NCHINI.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw Sabasaba Moshingi,( wa pili kulia) akiongoza zoezi la kugongesha glasi kuashiria upendo na furaha kwa wateja wa benki hiyo wakati hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika leo Jumatano Oktoba 6,2021 katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Diana Myonga.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw Sabasaba akimkabidhi cheti Mteja wa Benki hiyo  Goodluck Luhanjo, wakati hafla ya  uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa  Wateja iliyofanyika  leo Jumatano Oktoba 6,2021  katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM.

BENKI ya  Biashara Tanzania TCB  imesema hatua ya serikali kuweka mifumo imara  ya kifedha imezidi kuziboresha huduma za kifedha nchini ikiwemo kuongeza namba ya watu wanaotumia mifumo rasmi ya kifedha.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma Kwa wateja Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi amesema   Nia Yao ni kutoa huduma  hasa kuwapa fursa wateja wadogo wadogo ambao ndiyo  azma ya Serikali na Benki hiyo ya Biashara ya Tanzania

Moshingi amesema kuwa nia yao nikusogeza huduma rafiki kwa wateja wake ili kuhakikisha kuwa  kila mtanzania wa hali ya chini anatumia benki hiyo kwaajili ya uendeshaji wa biashara zao katika Nyanja tofauti.

Kwa upande wao baadhi ya wateja na watumiaji wa mifumo ya kibenki wamesema kitendo Cha baadhi ya taasisi kuanzisha huduma za kuwajali wastaafu imezidi kuongeza weledi hivyo wameishukuru Benki ya TCB kwakuendelea kuwaamini nakuwawezesha kupata mikopo kwa wakati na kwamashart rafiki

Previous articleHALMASHAURI YA JIJI DAR YAWAPA MAFUNZO WALIMU
Next articleTANZANIA KUPOKEA SHEHENA YA PILI YA CHANJO YA UVIKO 19 AINA YA SINOPHARM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here