Home LOCAL ALICHOKIAHIDI DR JPM HAPA CHATO RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

ALICHOKIAHIDI DR JPM HAPA CHATO RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Na: Mwandishi Wetu.

Ni Ujenzi wa Chuo cha VETA na Standi ya Kisasa Chato, Ujenzi wa Msikiti Kijiji Cha Amani Kwa kushirikiana na Taasisi ya Al Khekima pamoja na Kuendeleza Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato na Kuanzisha Mkoa wa Chato iwapo Vigezo Vinavyohitajika vitafikiwa.

Rais ameyasema hayo kwenye kilele cha Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Miaka 22 ya Kifo Cha Baba wa Taifa Mwal. Nyerere yaliyofanyika Chato Mkoani Geita. Raisamesema Miradi hiyo yote ataitekeleza na Wananchi wa Chato wasiwe na wasiwasi wowete.

Sambamba ma hayo Rais Samia amesema atahakisha miradi yote aliyoicha Rais John Pombe Magufuli Chato itaimalizia, miradi hiyo ni pamoja na uendelezaji wa ujenziwa hospitali ya rufaa Kanda ya Chato

Kitendo Cha Rais kuwahakikishia Wananchi wa Chato kukamilisha a kujenga Miradi hiyo ni ushahidi tosha kwamba anawapenda Wananchiwa Chato na kwa Vitendo anayaendeleza yaliyoachwa na hayati Dr John Pombe Magufuli Chato na Tanzania kwa ujumla

Kukamilika kwa Miradi hiyo Itasaidia kufungua kwa kasi fursa zilizopo Wilaya ya Chato kama vile Utalii, Uvuvi, biashara na Ufugaji ambazo zitainua Maisha ya Wananchi wa Chato

Kikubwa ni kwa Wananchi wa Chato kuendelea kua na Umoja na Mshikamano na zaidi kuunga Mkono jitihada za Rais kwa kufanya kazi kwa bidii na kutunza amani ya nchi yetu tuliyonayo.

*#Twende Pamoja*

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here