Home SPORTS YANGA YATUA NCHINI

YANGA YATUA NCHINI

Mwandishi wetu,Dar es Salaam.

MABINGWA wa mara 27 wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga wamewasili salama nchini  baada ya kutolewa katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha  Mkuu, Nasreddine Nabi leo Septemba 20 kimewasili salama katika ardhi ya Tanzania kikitokea nchini Nigeria.

Kikosi hicho ambacho kilikuwa kinapambana kupeperusha  bendera kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo Yanga na uongozi mzima  ulikuwa na lengo  kubwa ilikuwa ni kwenye kupindua meza kibabe mbele ya Rivers United kwa sababu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United hivyo walitakiwa kushinda mabao zaidi ya mawili.

Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rivers United pia jana na mchezo ulipokamilika walianza safari kurudi Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here