Home SPORTS YANGA YAAHIDI KUICHAPA KAGERA LEO

YANGA YAAHIDI KUICHAPA KAGERA LEO

 

Na: Mwandishi wetu, BUKOBA.

MABINGWA wa ngao wa jamii Yanga leo wanashuka dimbani dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba,Kagera.

Kikosi hicho inaingia kibabe uwanjani baada ya kuifunga Simba SC katika mchezo wa ngao ya jamii wikiend iliyopita.

Kikosi hicho kiliondoka juzi na wachezaji 25 kikiwa na matumaini ya ushindi leo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kikosi chao Yanga  kipo imara  kwa ajili ya mchezo huo.

Ni malengo yao kushinda  ili kuanza rasmi mbio za kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu huu wa 2021/22.

Hata hivyo alisema kuwa kikosi kina wachezaji wazuri ambao wamefanya mazoezi vyema kwa maelekezo ya kocha pia alibainisha kuwa wapo nyota ambao watakosekana katika mchezo wa leo kutokana na sababu mbalimbali. 

 Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na Said Ntibanzokiza, Mapinduzi Balama pamoja na Mukoko Tonombe pia ameweka wazi kwamba wanahitaji ushindi mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa wana rekodi nzuri wakiwa Kaitaba. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here