Home LOCAL WAZIRI AWESO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA

WAZIRI AWESO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan (kulia)katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Maji, Mtumba, jijini Dodoma.


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) katika kikao na Balozi wa India nchini kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Maji, Mtumba, jijini Dodoma.
Kikao cha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Srikanta kikiendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Maji, Mtumba, jijini Dodoma.


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na viongozi wa wizara wakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Maji, Mtumba, jijini Dodoma.

DODOMA.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa miji 28 wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 500 unaotarajiwa kuanza karibuni katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Maji, Mtumba, jijini Dodoma.

Waziri Aweso amemuomba Balozi Pradhan kuwezesha utekelezaji mzuri wa mradi mkubwa na muhimu wa kihistoria utakaoleta mapinduzi makubwa katika Sekta ya Maji Tanzania, unaotarajiwa kuanza punde uweze kukamilika haraka iwezekanavyo na ikiwezekana kabla ya muda uliopangwa.

Vilevile, ameishukuru Serikali ya India kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi wa maji wa Igunga, Nzega na Tabora kwa kutoa fedha za mkopo wa masharti nafuu kupitia Exim Bank ya India pamoja na wakandarasi kutoka India waliofanya kazi nzuri na kuwezesha mradi kukamilika kwa wakati na kiwango bora.

Pia, ameiomba India kuendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania kwenye Sekta ya Maji katika maeneo mbalimbali kwa dhumuni la kuinua kiwango cha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama nchini.

Aidha, Balozi Binaya Srikanta Pradhan amemuhakikishia Waziri Aweso ushirikiano mkubwa kutoka Serikali ya India kwenye maeneo mbalimbali ya kisekta pamoja na kuwajengea uwezo wataalam kwenye maeneo kukabiliana na upotevu wa maji, usimamizi na uendeshaji wa miradi na ujenzi wa miradi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga pamoja na viongozi wa idara wizarani hapo.

Previous articleBENKI YA NBC YAREJESHA TABASAMU KWA WATOTO.
Next articlePROF. MAKUBI AKUTANA NA MKURUGENZI WA KfW
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here