Home SPORTS WAKIMBIZA BAISKELI WAPATAO 100 KUANZA SAFARI YA KWENDA BUTIAMA KUMUENZI BABA WA...

WAKIMBIZA BAISKELI WAPATAO 100 KUANZA SAFARI YA KWENDA BUTIAMA KUMUENZI BABA WA TAIFA.

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

MSAFARA wa Baiskeli  unatarajiwa kuanza jumapili kutoka  Masaki mpaka Butiama  kwaajili ya  kuenzi miaka 22 tangu kifo cha Baba wa Taifa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari  Mkuu wa msafara wa huo Gabriel Landa amesema kuwa lengo la msafara huo ni kuenzi Baba wa Taifa kwa kuungana na watanzania wote.

Amesema kuwa msafara huo utaanzia katika  makazi yake Msasani Dar es Salaam na kuhitimisha Mwitongo,Butiama  kwa siku 14.

“Msafara huo ambao utatumia siku 14 kutoka Dar es Salaam mpaka Butiama  zenye umbali wa kilometa  zisipungua 1400 kupitia katika mikoa 10 wilaya 20 na kuhusisha  washiriki  wasiopungua 100”anasema.

Aliongeza kuwa watakuwa na washiriki zaidi ya 100 na wanategemea kuhitimisha msafara huko Mwitogo, Butuama wakiwa na washiriki zaidi ya 100 na ujumbe “changia dawati,tokomeza ujinga kwa maendeleo ya taifa”.

Aliongeza kuwa watanzania wataendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa mchango wake wa  juu ya mapambano ya uhuru waafrika kutoka kwa serikali ya kikoloni ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimoja bila kujali ukabila wala dini jambo linapelekea kudumisha mshikamano na amani kwa watanzania.

Alifafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa msafara huu wa Twende Butiama 2018,msafara huu umekuwa unahamasisha watanzania kuendeleza juhudi za baba wataifa  ikiwa ni pamoja na kupambana na maadui watatu  wa maendeleo ambao ni Ujinga, Maradhi  na umaskini.

Previous articleKMC YAJIPANGA KUICHAPA COASTAL UNION
Next articleAFISA MTENDAJI MKUU NFRA AWEKA WAZI UTEKELEZAJI MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA UHIFADHI NAFAKA KATIKA MAENEO NANE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here