Home SPORTS TFF YATANGAZA VIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA

TFF YATANGAZA VIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA

Na:Stella Kessy.

SHIRIKISHO  la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  limetangaza viingilio vya mchezo wa ngao ya jamii utakao wakutanisha watani wa jadi klabu za Simba na Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, 

Akizungumza leo na Vyombo vya Habari msemaji wa Shirikisho la Soka la Tanzania Cliford  Ndimbo,amasema viingilio vya mchezo huo ambao utaanza kutimua vumbi majira ya saa 11  kamili jioni.

Mzunguko  ni 10000 ikijumlishwa viti vya blue na kijani,  na Platinum hawauzi pamoja na VB 30000, VPC ,20000 na viti vya rangi ya chungwa 

Aliongeza Kuwa sehemu za kuuza tiketi zitatajwa kwa pamoja na siku ya kuanza kuuza.

Huku Kwa upande wa Yanga msemaji wao Hassani Bumbuli Amesema Kuwa kikosi kimeingia kambini na kipo tayari pamoja wachezaji ambao hawakucheza katika mechi za kimataifa watacheza pamoja na waliokuwa majeruhi wapo fiti kwa ajili ya kuibuka na ushindi.

“Ninachowaomba mashabiki wajitokeze Kwa wingi katika mchezo huu wakiwa na kijiamini  sababu kikosi kipo vizuri na wamejipanga vyema sababu mchezo huu Ndio kuanza kukusanya  pointi za ushindi”alisema.

Kwa upande wa msemaji wa simba Ezekiel Kamwaga alisema kuwa kikosi Cha Simba kilikuwa na mapumziko ya siku mbili Baada ya kumaliza mechi dhidi ya TP Mazembe na Leo wanawasili kambini.

“Ninachoomba mashabiki wajitokeze Kwa wingi katika mchezo huo muhimu kwa Simba lengo ni kuona kikosi chao kikiwa na mwanzo mzuri dhidi ya watani wetu”alisema.

Previous articleGGML YAWATAKA WADAU WA SEKTA YA MADINI KUYATUMIA MAONESHO YA MADINI KUPATA ELIMU
Next articleSERIKALI KUTUMIA RASILIMALI ZA NCHI KUINUA UCHUMI WA WATANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here