Home SPORTS STARS YAIBUKA NA USHINDI WA 3-2 DHIDI YA MADAGASCAR.

STARS YAIBUKA NA USHINDI WA 3-2 DHIDI YA MADAGASCAR.

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KIKOSI Cha timu ya Taifa  ya Tanzania kimeibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Madagascar katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana 2-2, Taifa Stars ikitangulia kwa mabao ya kiungo wa Simba SC ya nyumbani, Erasto  Nyoni dakika ya tatu tu kufuatia mshambuliaji wa Wydad Athletic ya Morocco, Simon  Msuva kuangushwa kwenye boksi.

Kiungo wa Maccabi Tel Aviv ya Israel, Novatus Dismas Miroshi akaifungia bao la pili Taifa Stars dakika ya 26 akimalizia kazi nzuri ya Nahodha na mshambuliaji wa Royal Antwerp ya au Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta.

Hata hivyo Madagascar iliamka na kupata  mabao ya winga wa Suphanburi FC ya Thailand, Njiva Tsilavina Martin Rakotoharimalala dakika ya 36 na beki wa Lorient ya Ufaransa, Thomas Fontaine dakika ya 45 na ushei. 

Katika dakika za 52 Feisal  Abdallah aliyefunga bao la ushindi.

Hata hivyo Kwa ushindi huo, Tanzania inapanda kileleni Kundi J ikifikisha pointi nne baada ya mechi mbili, kufuatia sare ya 1-1 na wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kwanza Alhamisi iliyopita.

Hata hivyo Benin inafuatia ikiwa na pointi nne pia, wakati DRC ni ya tatu kwa pointi zake mbili na Madagascar hawana pointi baada ya kufungwa nyumbani na ugenini mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here